Huo ni mwanzo mzuri kwa kocha Muingereza Dylan Kerr Simba SC, kwani sasa Wekundu wa Msimbazi nao wamo kwenye mbio za ubingwa.
Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Mzimbabwe Justuce Majabvi dakika ya 27 baada ya krosi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuzua kizazaa langoni mwa Mgambo.
Mgambo walikosa bao la wazi dakika ya 19 baada ya shuti la Salim Aziz Gillah kupaa juu kidogo ya lango.
Said Ndemla alikaribia kufunga dakika ya 35 kwa kichwa akimaizia krosi ya Hassan Kessy lakini mpira ukatoka nje kidogo ya lango.
Mgambo tena wakakosa bao la wazi baada ya shuti la Nassor Gumbo aliyeingia akichukua nafasi ya Salim Gillah kugonga mwamba na kurudi uwanjani dakika tano baaadye.
Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliifungia Simba SC bao la pili dakika ya 73 akimalizia pasi Ibrahim Hajibu baada ya gonga safi baina yao.
Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba SC baada ya awali kuifunga African Sports 1-0, bao pekee la Kiiza.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika, Mohamed Hussein, Hassan Ramadhani, Murushid Juuko, Hassan Isihaka, Justuce Majabvi, Awadh Juma, Said Ndemla/Abdoulaye Pape N’daw dk69, Mussa Mgosi/Ibrahim Habib dk67, Mwinyi Kazimoto/Hamisi Kiiza dk46 na Peter Mwalianzi.
Mgambo JKT; Said Abdi, Bashiru Chanache, Salim Mlima, Salim Kipaga, Ramadhani Malima/Athanas Chacha, Bakari Mtama, Salim Gillah, Mohammed Samatta, Helbert Charles, Fullu Zulu Maganga/Bolly Shaibu dk68 na Chande Magoja.
****
YANGA SC
imeendelea kung’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa
mabao 3-0 Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.
Mabingwa hao watetezi, sasa wanafikisha pointi sita na mabao matano, baada ya awali kushinda pia nyumbani 2-0 dhidi ya Coastal Union.
Hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Mkongo, Mbuyu Twite dakika ya 27 baada ya kipa wa Prisons, Mohammed Yussuf kushindwa kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa na Simon Msuva, kufuatia Deus Kaseke kuangushwa nje ya boksi.
Mrundi Amissi
Tambwe aliifungia Yanga SC bao la pili dakika 45 akiumalizia mpira
uliopanguliwa na kipa wa Prison, Yussuf baada ya mpira wa adhabu wa kiungo wa
Rwanda, Haruna Niyonzima kufuatia Msuva tena kuangushwa.
Mshambiliaji wa Prisons Jeremiah Juma alipoteza nafasi nzuri ya kufunga kipindi cha kwanza baada ya kupia juu la lango.
Kipindi cha pili, kocha wa Prisons, Salum Mayanga
alianza kwa kumpumzisha kipa Yussuf na kumuingiza Aron Kalambo
Refa Alex Mahagi wa Mwanza alimtoa kwa kadi nyekundu James Josephat dakika ya 59 baada ya kumdondosha Msuva kwenye boksi na Mzimbabwe Donald Ngoma akaifungia Yanga SC bao la tatu kwa penalti dakika ya 60.
Refa Alex Mahagi wa Mwanza alimtoa kwa kadi nyekundu James Josephat dakika ya 59 baada ya kumdondosha Msuva kwenye boksi na Mzimbabwe Donald Ngoma akaifungia Yanga SC bao la tatu kwa penalti dakika ya 60.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Haji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke/Salum Telela dk66
Simon Msuva, Haruna
Niyonzima Geoffrey Mwashiuya dk79, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk84, Donald
Ngoma na Deus Kaseke.
Prisons: Mohammed Yussuf/ Aron Kalambo dk46, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, James Josephat, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambert Sabianka, Juma Seif, Mohammed Mkopi/Cosmas Ader dk47, Boniface Hau Ally Manzi dk64 na Jeremiah Juma.
FT YANGA 3 : 0 T.PRISONS
FT MGAMBO JKT 0 : 2 SIMBA SC
MAJIMAJI 0 : 0 KAGERA
SUGAR
FT MBEYA CITY 3 : 0 JKT RUVU
FT STAND UNITED 0 : 2 Azam
FC
TOTO AFRICANS 1 : 2 MTIBWA
SUGAR
NDANDA FC 0 : 0 COASTAL
UNION
FT MWADUI FC 1 : 0 AFRICAN SPORT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni