Mbwana Samatta alifunga mabao matatu peke yake Mazembe ikishinda 5-0 mwishoni mwa wiki
TP
Mazembe itamenyana na El Merreikh ya Sudan katika Nusu Fainali ya Ligi
ya Mabingwa Afrika, mchezo wa kwanza ukichezwa Septemba 25, mwaka huu
mjini Khartoum na marudiano Oktoba 2 mjini Lubumbashi.
Huo
ni mtihani mkubwa kwa Mazembe, kwani imekuwa ikisumbuliwa mno na timu
za Sudan- katika hatua ya makundi mwaka huu ilipangwa na El Hilal na
haikushinda hata mchezo mmoja.
Mchezo
wa kwanza Lubumbashi ililazimishwa sare kabla ya kufungwa 1-0 mchezo wa
marudiano Sudan- na saa wanakutana na timu ambayo inaaminika ndiyo bora
zaidi nchini humo.
Nusu
Fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa kati ya El Hilal ya
Sudan na USM Alger ya Algeria, nao pia mechi ya kwanza itakuwa Septemba
25 na marudiano Oktoba 2, mwaka huu.
Rais
wa TP Mazembe, Moise Katumbi Chapwe amefurahia ushindi wa 5-0 katika
mchezo wa mwisho mwishoni mwa wiki dhidi ya Moghreb Tetouan YA Morocco
na kuongoza Kundi A, Mbwana Ally Samatta wa Tanzania akifunga mabao
matatu.
“Kabla
ya mchezo, nilitarajia mabao mawili kwa Mbwana Samatta. Ni mchezaji
babu kubwa ambaye aliibuka baada ya kipindi kigumu alichopitia.
Wakati
wote nawaamini wachezaji, kwa sababu kuna wakati wanakuwa hawajisikii
vizuri. Mbwana Samatta amefunga, tunatarajia kufanya vizuri
zaidi,”amesema katumbi.
Ikumbukwe,
safari ya Merreikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilianzia Dar es
Salaam ambako ilifungwa 2-0 na Azam FC, kabla ya kwenda kushinda 3-0
nyumbani katika mchezo wa marudiano na kusonga mbele.
Mbwana Samatta alifunga mabao matatu peke yake Mazembe ikishinda 5-0 mwishoni mwa wiki |
TP Mazembe itamenyana na El Merreikh ya Sudan katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo wa kwanza ukichezwa Septemba 25, mwaka huu mjini Khartoum na marudiano Oktoba 2 mjini Lubumbashi.
Huo ni mtihani mkubwa kwa Mazembe, kwani imekuwa ikisumbuliwa mno na timu za Sudan- katika hatua ya makundi mwaka huu ilipangwa na El Hilal na haikushinda hata mchezo mmoja.
Mchezo wa kwanza Lubumbashi ililazimishwa sare kabla ya kufungwa 1-0 mchezo wa marudiano Sudan- na saa wanakutana na timu ambayo inaaminika ndiyo bora zaidi nchini humo.
Nusu Fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa kati ya El Hilal ya Sudan na USM Alger ya Algeria, nao pia mechi ya kwanza itakuwa Septemba 25 na marudiano Oktoba 2, mwaka huu.
Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi Chapwe amefurahia ushindi wa 5-0 katika mchezo wa mwisho mwishoni mwa wiki dhidi ya Moghreb Tetouan YA Morocco na kuongoza Kundi A, Mbwana Ally Samatta wa Tanzania akifunga mabao matatu.
“Kabla ya mchezo, nilitarajia mabao mawili kwa Mbwana Samatta. Ni mchezaji babu kubwa ambaye aliibuka baada ya kipindi kigumu alichopitia.
Wakati
wote nawaamini wachezaji, kwa sababu kuna wakati wanakuwa hawajisikii
vizuri. Mbwana Samatta amefunga, tunatarajia kufanya vizuri
zaidi,”amesema katumbi.
Ikumbukwe, safari ya Merreikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilianzia Dar es Salaam ambako ilifungwa 2-0 na Azam FC, kabla ya kwenda kushinda 3-0 nyumbani katika mchezo wa marudiano na kusonga mbele.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni