RAIS
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema timu ya
taifa ya wanawake, Twiga Stars imekwama kwenda Kongo- Brazzavile kwenye
Michezo ya Afrika kutokana na kutopatiwa usafiri na Serikali.
Akizungumza
na moja ya chanzo cha habari leo Malinzi amesema tangu juzi viongozi
wa TFF wamekuwa wakishinda ofisi za Wizara ya Habari Utamaduni na
Michezo kufuatilia tiketi, lakini hawajafanikiwa.
“Ni
hatari sana iwapo timu hii haitakwenda Kongo-Brazzavile, tunaweza
kufungiwa kwenye mashindano yote ya kimataifa, kwa kweli tupo kwenye
wakati mgumu,”amesema Malinzi.
Rais
huyo wa TFF, amesema wao waliipeleka timu kambini Zanzibar na tangu
awali inafahamika suala la kuisafirisha timu kwenda Kongo-Brazzavile ni
la Serikali.
“Hii
ni sehemu ya Michezo ya Olimpiki na kama unavyojua wanamichezo wote wa
Tanzania waliokwenda huko wamesafirishwa na Serikali, hivyo hili nalo ni
jukumu lao,”amesema Malinzi.
Michezo
ya Afrika (All Africa Games) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho na
Twiga Stars itafungua dimba na Ivory Coast Septemba 6, kabla ya
kumenyana na Nigeria Septemba 9 na kumaliza mechi za kundi lake kwa
kumenyana na wenyeji Kongo-Brazzavile Septemba 12.
Timu mbili kutoka kundi A zitaungana na timu mbili nyingine kutoka kundi B kucheza hatua ya nusu fainali.
Habari
zinasema Mawaziri wote wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Dk,
Fenela Mukangara na Juma Nkamia wapo ‘bize’ na kampeni za Ubunge na hilo
ndilo linasababisha kukwama kwa Twiga Stars.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatano, 2 Septemba 2015
TWIGA STARS WAKWAMA KWENDA KONGO-BRAZZAVILE KWENYE MICHEZO YA AFRIKA .........
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni