KOCHA Brendan Rodgers amefukuzwa kazi Liverpool usiku huu kufuatia matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya England.
Raia
huyo wa Ireland Kaskazini aliambiwa baada ya sare ya 1-1 na Everton leo
kwamba miaka yake mitatu na nusu ya kuanya kazi Anfield imetosha.
Rodgers,
ambaye timu yake imeshinda mechi moja tu kati ya tisa zilizopita ndani
ya dakika 90, amepewa taarifa hizo kwa simu juu ya kufukuzwa kwake.
Rodgers
amekuwa kocha wa Wekundu hao tangu Juni mwaka 2012 alipotua akitokea
Swansea City na alisaini Mkataba mpya wa miaka minne zaidi ya mwaka
mmoja uliopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni