KIUNGO wa Manchester
City, Samir Nasri amesisitiza kuwa hakuna kitu chochote kinachoweza
kumfanya kuja kuichezea tena timu ya taifa ya Ufaransa.
Nyota huyo wa
zamani wa klabu za Marseille na Arsenal mara ya mwisho kuitumikia nchi
yake ilikuwa mwaka 2013 lakini aliamua kuachana na soka la kimataifa
baada ya kuachwa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 pamoja na
kuwa sehemu muhimu katika kikosi cha City kilichonyakuwa taji la Ligi
Kuu msimu wa 2013-2014.
Nasri amekuwa na historia mbaya na Ufaransa
kufuatia kuachwa pia katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 kabla
ya kusimamishwa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo kwa kuzozana na
wanahabari kufuatia kutolewa kwa Ufaransa katika hatua ya robo fainali
ya michuano ya Euro 2012.
Akihojiwa Nasri amesema hata kama baba yake
ndio atakuwa kocha Ufaransa hatathubutu kurejea kuitumikia timu hiyo
kutokana na mambo waliyomfanyia.
Kiungo huyo amesema baada ya michuano
ya Euro 2012 alitaka kuacha lakini baba yake alimwambia anatakiwa
kucheza Kombe la Dunia na baada ya hapo alijaribu kuwa vizuri huku
akijituma katika klabu yake lakini aliachwa.
Nasri aliendelea kudai kuwa
jambo lilimuudhi na akiwa kama binadamu akaamua kuchukua maamuzi na
kutofiria masuala hayo na badala yake kuongeza nguvu katika klabu yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni