Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amemmwagia sifa kiungo wake mshambuliaji kutoka Brazil, Willian kwamba ni mfano wa kuigwa kikosini kutokana na kujitolea kwake kuisaidia timu.
Willian ambaye alihusika katika goli la kwanza baada ya kupiga krosi iliyosababisha mchezaji Aleksander Dragovic wa Dynamo Kiev kujifunga mwenyewe, pia aliifungia timu yake goli la ushindi mara baada ya kupiga faulo nzuri iliyojaa moja kwa moja golini na kuipa Chelsea ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Dynamo Kiev.
Akiongea mara baada ya mchezo, Mourinho amesema kuwa kuna wachezaji ambao pamoja na timu kupitia kipindi kibaya lakini wao bado wanacheza katika morali na uwezo ule ule na mtu huyo ni Willian.
Mourinho anasema kuwa wakati mwingine ni vizuri kusifia mtu anapofanya vizuri huku akisisitiza kuwa pamoja na wachezaji wengine kucheza pia vizuri lakini Willian alikua katika fomu nzuri sio tu usiku wa jana bali tangu kuanza kwa msimu huu.
Aidha Edin Hazard alianzia katika benchi kitu ambacho Mourinho anakielezea kama afya katika benchi kutokana na alichokisema kuwa alikua na machaguo ya kutosha huku akijinasibu kuwa timu iliongeza kujiamini wakati Eden Hazard na Pedro Rodriguez walikua wakiingia uwanjana huku kila mmoja akijua kuwa wachezaji hao wana uwezo wa kubadili matokeo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni