KIUNGO wa Chelsea, Cesc 
Fabregas amekanusha tuhuma za vyombo vya habari kuwa ndiye kinara wa 
kutengeneza mgomo katika vyumba vya kubadilisha nguo kumpinga meneja wao
 Jose Mourinho. 
Blog moja ya michezo nchini Uingereza imedai Fabregas 
ndio alikuwa kinara wa mgomo baridi katika klabu hiyo ambayo ndio 
mabingwa watetezi wa Ligi Kuu. 
Akitumia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa
 twitter, Fabregas alikanusha taarifa hizo zilizozagaa dhidi yake akidai
 kuwa anafurahia maisha katika klabu hiyo na amekuwa na mahusiano mazuri
 na Mourinho. 
Kiungo huyo aliendelea kudai kuwa kuna watu wachache 
kutoka nje wanataka kuiyumbisha klabu lakini anaamini wanaweza kuyapita 
magumu hayo na kuimarika kama zamani. 
Chelsea ambao wamepoteza michezo 
yao sita kati ya 11 waliyocheza msimu huu wanashikilia nafasi ya 15 
katika msimamo wa ligi.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni