Nahodha Wayne Rooney akiruka kichwa baada ya kuifungia Manchester United jana
MANCHESTER zote, City na United zimeshinda mechi zao za Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo.
United imeibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi
Shukrani kwake Nahodha, Wayne Rooney aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 79 katika mchezo huo wa Kundi B Uwanja wa Old Trafford.
Mchezo mwingine wa Kundi B, PSV imeshinda nyumbani mabao 2-0 dhidi ya VfL Wolfsburg, mabao ya Jurgen Locadia dakika ya 55 na Luuk de Jong aliyejifunga dakika ya 86 Uwanja wa Philips.
Man City imepata ushindi ‘mtamu’ ugenini wa mabao 3-1 dhidi ya Sevilla katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Ramon-Sanchez Pizjuan, mabao yake yakifungwa na Raheem Sterling dakika ya nane, Fernando Luiz Rosa dakika ya 11 na Wilfried Bony dakika ya 36, huku la wenyeji likifungwa na Benoit Tremoulinas dakika ya 25.
Mchezo mwingine wa Kundi D, Borussia Monchengladbach imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Juventus, bao lao likifungwa na Fabian Johnson dakika ya 18, kabla ya Stephan Lichtsteiner kuwasawazishia Kibibi Kizee cha Turin dakika ya 44 Uwanja wa Borussia-Park.
Raheem Sterling akishangilia baada ya kuifungia Man City jana
Bao pekee la Jose Ignacio Fernandez Iglesias dakika ya 35 limeipa ushindi mwembamba wa 1-0 Real Madrid Uwanja wa Santiago Bernabeu dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa Kundi A.
Mchezo mwingine wa Kundi A, Shakhtar Donetsk imeifumua 4-0 Malmo FF Uwanja wa Arena Lviv, mabao ya Olexandr Gladkiy dakika ya 29, Darijo Srna kwa penalti dakika ya 48, Eduardo Alves da Silva dakika ya 55 na Alex Teixeira dakika ya 73.
Benfica imeshinda 2-1 nyumbani dhidi ya Galatasaray katika mchezo wa Kundi C, mabao yake yakifungwa na Jonas Goncalves Oliveira dakika ya 52 na Anderson Luis da Silva dakika ya 67, huku la wageni likifungwa na Lukas Podolski dakika ya 58 Uwanja wa Estadio da Luz.
Beki wa PSG, Thiago Silva akipambana na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid jana
Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Astana imelazimishwa sare ya 0-0 na Atletico Madrid Uwanja wa Astana Arena.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Astana imelazimishwa sare ya 0-0 na Atletico Madrid Uwanja wa Astana Arena.
Ligi ya Mabingwa inaendelea leo, Bayern Munich wakiwakaribisha Arsenal Uwanja wa Allianz Arena katika mchezo wa Kundi F, Roma na Bayer 04 Leverkusen Uwanja wa Olimpico Kundi E, Chelsea na Dynamo Kyiv Uwanja wa Stamford Bridge Kundi G.
Mechi nyingine za leo ni kati ya Maccabi Tel Aviv na FC Porto Uwanja wa Bloomfield Kundi G, Lyon na Zenit St Petersburg Uwanja wa Stade de Gerland Kundi H, KAA Gent na Valencia CF Uwanja wa Ghelamco Arena Kundi H, Olympiakos na Dinamo Zagreb Georgios Uwanja wa Karaiskakis Kundi F na Barcelona na BATE Borisov Uwanja wa Camp Nou Kundi E.
MATOKEO NA RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA;
Novemba 3, 2015
Shakhtar Donetsk 4-0 Malmo FF
B. Monchengladbach 1-1 Juventus
Benfica 2-1 Galatasaray
Real Madrid 1-0 Paris Saint-Germain
Sevilla 1-3 Manchester City
PSV 2-0 VfL Wolfsburg
Manchester United 1-0 CSKA Moscow
FC Astana 0-0 Atletico de Madrid
Msimamo wa makundi yote ya timu ambazo zilicheza mechi zao usiku wa Jumanne, November 3, 2015
Leo; Novemba 4, 2015
Roma Vs Bayer 04 Leverkusen (Saa 4:45 Usiku)
Bayern Munich Vs Arsenal (Saa 4:45 Usiku)
Chelsea Vs Dynamo Kyiv (Saa 4:45 Usiku)
Maccabi Tel Aviv Vs FC Porto (Saa 4:45 Usiku)
Lyon Vs Zenit St Petersburg (Saa 4:45 Usiku)
KAA Gent Vs Valencia CF (Saa 4:45 Usiku)
Olympiakos Vs Dinamo Zagreb (Saa 4:45 Usiku)
Barcelona Vs BATE Borisov (Saa 4:45 Usiku)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni