Matola akiwa na kocha mkuu wa zamani wa Simba Koponovic
KOCHA
Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Abdallah Matola amejiuzulu nafasi hiyo
kutokana na kile alichodai kutolelewana na Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan
Kerr.
Akizungumza, Matola amesema kwamba
amefikia uamuzi huo baada ya kuona maelewano na bosi wake huyo yanazidi
kuwa magumu kila kukicha.
Seleman Matola katika benchi la ufundi la Simba
“Ni jambo la muda mrefu, huyu kocha hasikilizi ushauri wangu, imefikia sasa ananichukia na kazi haziendi tena. Sasa nimeona ili kuepusha matatizo zaidi, nimuachie yeye timu,”amesema Matola.
Matola
amesema kwamba haoni mwelekeo wowote mzuri kwa Simba SC chini ya kocha
huyu Muingereza ambaye hasikilizi ushauri, ndiyo maana ameamua kujitoa.
Suleiman Matola (kulia) ameachia ngazi Simba SC baada ya kutofautiana na bosi wake, Dylan Kerr (kushoto).
“Nimekutana
na uongozi, nimewaambia juu ya uamuzi wangu, wakanisihi sana nisifanye
hivyo, lakini nikashikilia msimamo wangu. Wakaniambia hata nirudi
kufanya kazi timu za vijana, lakini nikawaambia nitajifikiria
kwanza,”amesema Matola.
Juhudi
za kumpata Kerr kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa na hakuna
kiongozi wa Simba SC aliyepatikana mapema jioni hii kuelezea sakata
hilo.
Historia
ya Matola ndani ya Simba SC inaanzia mwaka 2000 alipojiunga nayo kama
mchezaji akitokea Kagera Stars (sasa Kagera Sugar) na aliichezea timu
hiyo hadi mwaka 2005 alipohamia Super Sport United ya Afrika Kusini.
Matola alirejea Simba SC mwaka 2007 na kucheza kwa msimu mmoja kabla ya kustaafu moja kwa moja.
Kuanzia
mwaka 2010 amekuwa kocha wa timu za vijana za Simba SC ambako baada ya
kufanya vizuri akapandishwa kuwa Kocha Msaidizi, akianza kufanya kazi na
Mcroatia Zdravko Logarusic, baadaye Mzambia, Patrick Phiri, Mserbia,
Goran Koponovic na huyu wa sasa Kerr.
Seleman Matola akiwa na Patrick Phir kocha mkuu wa zamani wa Simba
Seleman Matola akiwa na Patrick Phir kocha mkuu wa zamani wa Simba
Haijawahi
kutokea Matola akatofautiana na kocha yeyote kati aliyofanya nao kazi
awali – na Muingereza huyu anakuwa wa kwanza kutofautiana na Nahodha wa
zamani wa Simba SC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni