Kwa kuwa uwanja huo si rasmi na hauna uzio wala huduma muhimu ikiwemo vyoo, waandaaji wa ligi hiyo, kamati ya muda ya ZFA wamejikuta wakipata hasara kwani hakuna kiingilio cha fedha kilichowekwa kwa watazamaji.
Na katika mchezo wa ufunguzi jana, JKU makamu bingwa msimu uliopita, waliilaza Mafunzo mabao 2-1.
Kamisaa wa mchezo Ramadhani Ibada Kibo, akiwaongoza waamuzi wa mpambano huo kurudi uwanjani kuanza kipindi cha pili, baada ya kupumzika katika kichaka pembezoni mwa uwanja.
Mafunzo ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo na wawakilishi wa Zanzibar kweli Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, wakati JKU watashiriki Kombe la Shirikisho.
Wakati wa mapumziko, waamuzi wa mtanange huo walilazimika kujipumzisha kwenye kichaka kinachozunguka uwanja huo.
Mgeni rasmi katika mchezo huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, alishuhudia hali hiyo, na kuahidi kuchukua hatua ya kuiomba Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Michezo, kuruhusu uwanja wa Amaan utumike kwa ligi hiyo ya nchi.
Wachezaji wa JKU (nyekundu) na Mafunzo (kijani) wakipambana katika mechi ya ufunguzi Ligi Kuu ya Zanzibar jana uwanja wa Bweleo
Uwanja wa pili wa Mao Tse Tung ambao ndio unaosaidia uwanja wa Amaan, kwa sasa umeshabomolewa kusubiri ujenzi mpya unaofadhiliwa na Jamhuri ya Watu wa China.
Mabao yote ya JKU katika pambano hilo yalifungwa na Mohammed Abdalla dakika ya 46 na 66, huku lile la Mafunzo likiwekwa kimiani na Abdulrahim Mohammed 'Mbambi' dakika ya 79.
Ligi hiyo inaendelea tena leo uwanjani hapo kwa kuwakutanisha maafande wa JWTZ, timu ya Kipanga na mabaharia wa KMKM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni