Chanzo: Bin Zubeir
MSHAMBULIAJI
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Ramadhani Mgunda ameteuliwa
kuwa Msaidizi namba moja wa Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden'
katika kikosi cha timu ya Tanzania Bara, 'Kilimanjaro Stars'
kitakachoshiriki michuano ya CECAFA Chellenge baadaye mwezi huu mjini
Addis Ababa, Ethiopia.
Kilimanjaro Stars inashiriki michuano hiyo mikongwe kabisa barani Afrika, ambapo jumla ya nchi 12 wanachama wamedhibitisha kushiriki michuano hiyo itakayomalizika Disemba 6 mwaka huu.
Nchi zingine zinazoshiriki michuano hiyo ni tofati na Tanzania bara ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudani, Sudani Kusini, Uganda na Zanzibar.
Kibadeni mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, na timu ya Taifa Tanzania, ni kocha mwenye leseni B, ambapo ameshafundisha vilabu vingi chini kwa mafanikio ikiwemo kuifiksha klabu ya Simba katika hatua ya fainali ya kombe la Washindi mwaka 1993.
Kocha Kibadeni ni mkurugenzi wa ufundi wa kituo cha mchezo cha KISA kilichopo Chanika, amewahi pia kuzifundisha timu za Kagera Sugar, JKT Ruvu.
Kocha msaidizi wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda ana leseni B ya CAF, zamani alikuwa mshambuliaji wa timu ya Coastal Union na timu ya Taifa Tanzania, pia aliweza cheza soka la kulipwa katika klabu ya Nahd nchini Oman.
Mgunda amewahi kuifundisha timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, timu ya mkoa wa Tanga, kocha wa kituo cha vijana cha mkoa wa Tanga.
Aidha, Mgunda ni mkufunzi wa msaidizi wa mafunzo ya makocha ngazi pevu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni