Messi ndiye mchezaji anayepewa kipaumbele na watu wengi wakiamini huenda akachukua tuzo hiyo kutokana na mafanikio aliyoyapata na timu ya Barcelona ambayo aliisadia kuchukua makombe matatu katika msimu uliopita (treble) wakati mpinzani wake Ronaldo ambaye anatetea taji lake akipewa nafasi ndogo kwenye tuzo hizo.
Endapo kama Messi akichukua tuzo hiyo kwenye sherehe zitakazo fanyika mjini Zurich mwezi January 11, 2016, hilo itakuwa tuzo yake ya 5 ya mchezaji bora wa dunia na atakuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo.

Mwaka huu Messi ameungana na mchezaji mwenzake kwenye timu ya Barcelona Neymar, ambaye amefunga magoli 10 kwenye kombe la UEFA Champions League, ikiwemo bao muhimu kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Juventus kule Berlin.
Mbrazili huyo pia alishika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa La Liga msimu uliopita akifunga magoli 22 na kwa sasa yeye ndiye anayeongoza kwa ufungaji kwenye ligi hiyo akiwa tayari ameshafunga magoli 14.
Kwa upande wa makocha walioingia kwenye tatu bora ni Luis Enrique wa Barcelona, Pep Guardiola wa Bayern Munich na Jorge Sampaoli wa timu ya taifa ya Chile
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni