STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 30 Novemba 2015

TANZANIA BARA "OUT" CECAFA CHALLENGE, YAPIGWA KWA MATUTA NA MWENYEJI

TANZANIA Bara imetolewa katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 na wenyeji Ethiopia, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
 
Katika mchezo huo wa Robo Fainali uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Tanzania Bara walikuwa wa kwanza kupata kupata bao liliofungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyemalizia krosi ya Deus Kaseke dakika ya 25.
Ethiopia walisawazisha kwa penalti iliyofungwa na Nahodha wake, Panom Gathouch baada ya Mohammed Naser kuangushwa na Shomary Kapombe dakika ya 57.

Mpaka dakika 90 kumalizika timu hizo zilikuwa sare ya kufungana 1-1, na ndipo ilipokuja changamoto ya mikwaju ya penalti. 
Beki Shomary Kapombe na kiungo Jonas Mkude walikwenda kupoteza penalti zao, wakati waliofunga kwa upande wa Kilimanjaro Stars ni kiungo Himid Mao, mshambuliaji Bocco na beki Hassan Kessy.

 
Waliofunga penalti za Ethiopia ni Panon Gathouch, Mohammed Naser, Ashalew Tamene na Behaylu Girima.  

 
Katika Robo Fainali ya Kwanza, Uganda imeifunga 2-0 Malawi mabao ya Farouk Miya na Ceasar Okhuti na sasa itakutana na Ethiopia katika Nusu Fainali, wakati Kili Stars inarejea nyumbani Dar es Salaam.

 
Kikosi cha Tanzania Bara kilikuwa; Said Mohamed, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Kevin Yondan, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Simon Msuva, Himid Mao, John Bocco, Said Ndemla na Deus Kaseke.

 
Ethiopia; Abel Mamo, Yared Bayeh, Aschalew Tamane, Anteneh Tesfaye, Aschalew Girma, Eliyas Mamo, Zekariyas Tuji, Gothuoch Panom, Beneyam Belay, Mohammed Naser na Bereket Yisshak.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox