Nigeria wakishangilia ubingwa wao
TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Nigeria, Golden Eaglets imetwaa ubingwa wa Dunia wa vijana wa umri wa huo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mali jana nchini Chile.
Ushindi huo unamaanisha kwamba Nigeria imetetea taji lao ililolitwaa miaka miwili iliyopita Falme za Kiarabu (UAE).
Mabao ya haraka haraka ya kipindi cha pili ya Victor Osimhen na Funsho Bamgboye yalitosha kukihakikishia taji hilo kikosi cha Emmanuel Amuneke, hilo likiwa taji la tano la dunia kwa U17.
Hii ni mara ya kwanza Nigeria wanatwaa taji hilo nje ya Asia, baada ya mataji yao ya awali kubeba China mwaka 1985, Japan mwaka 1993, Jamhuri ya Korea mwaka 2007 na UAE mwaka 2013.
Kelechi Nwakali,mchezaji bora wa michuano
Victor Osimhen kushoto ndie mfungaji bora wa michuano akimaliza kwa kufunga magoli10
Adidas Golden Ball
Adidas Golden Boot
Adidas Golden Glove
MABINGWA WA KOMBE HILI:
Team | Titles | Runners-up | Third-place | Fourth-place | Medals | |||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nigeria | 5 (1985, 1993, 2007, 2013, 2015) | 3 (1987, 2001, 2009) | 8 | |||||
Brazil | 3 (1997, 1999, 2003) | 2 (1995, 2005) | 1 (1985) | 1 (2011) | 6 | |||
Ghana | 2 (1991, 1995) | 2 (1993, 1997) | 1 (1999) | 1 (2007) | 5 | |||
Mexico | 2 (2005, 2011) | 1 (2013) | 1 (2015) | 3 | ||||
Soviet Union | 1 (1987) | 1 | ||||||
Saudi Arabia | 1 (1989) | 1 | ||||||
France | 1 (2001) | 1 | ||||||
Switzerland | 1 (2009) | 1 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni