Kocha wa Bayern Munich Pep Guadiola kupitia kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Karl-Heinz Rummenigge imesema kuwa kocha huyo ataweka hadharani mustakabali wa wapi atakako kuwepo baada ya msimu huu kwisha kabla ya sikukuu ya Christmas msimu huu.
Rummenigge amesema Guadiola atatoa surprise ya Christmas na kwamba watu wasubiri kuona wapi ataelekea kocha huyo ama ataongeza mkataba na klabu yake ya sasa ya Bayern Munich.
Guadiola ambaye amebakiza hadi mwezi Juni mwakani kumaliza mkataba wake na klabu yake ya Bayern, amekua akihusishwa sana na taarifa za kuhamia klabu za Manchester City na Chelsea za nchini England.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni