Mtanzania Mbwana Samatta ameiweka klabu
yake ya TP Mazembe katika nafasi nyingine ya kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa
Afrika baada ya kufunga bao muhimu.
Licha ya kuwa ugenini, TP Mazembe
ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Rainford Kalaba katika dakika ya 27 lakini
dakika ya 45 Mzambia huyo akatolewa kwa kadi nyekundu.
Beki
wa USM Alger akimuangusha mshambuliaji Mtanzania wa TP Mazembe katika
fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa jana Uwanja wa
Omar Hamadi de Bologhine mjini Algiers Pigo hilo lilisababisha penalti .
Kipindi cha pili, TP
Mazembe walionyesha kuwa makini wakilinda lbao lakini walimtumia Samatta
kuendelea kuwasumbua walinzi wa USM Alger.
Dakika ya 68, Hocine
El Orfi alilambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu.
Dakika ya 79, Samatta
akafanya yake baada ya kufunga bao la pili na kuiweka Mazembe katika nafasi
nzuri kabla ya mechi ya marudiano Novemba 8 mjini Lubumbashi.
Hata hivyo wenyeji walionekana kutokata tamaa hadi walipopata bao moja katika dakika ya 88 kupitia kwa Mohammed Seguer.
TIZAMA VIDEO YA MAGOLI:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni