Fainali za michuano ya vilabu bingwa Duniani imemalizika kule nchini Japan katika uwanja wa Yokohama mjini Yokohama na kushuhudia Barcelona waki ibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya mabingwa wa Amerika ya kusini River Plate inayotoka nchini Argentina.
Messi aliaanza kuifungia Barcelona goli la kwanza mnamo dakika ya 37 kisha Suarez mnamo kipindi cha pili akafunga goli la pili dakika ya 49 na 68
Matokeo hayo Barcelona wameandika historia ya kuwa klabu iliyotwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi ikiwa ni mara tatu, mara ya kwanza ni mwaka 2009 kisha 2011 na 2015 na kuwaacha Corinthians wakiwa wamechukua mara mbili.
lakini pia magoli mawili ya Suarez yamemfanya kuwa mfungaji bora katika mashindano haya ya 2015 na wa muda wote katika mashindano hayo tangu kuanzishwa kwake 2000 akiwa na magoli 5 katika michezo 2 akishiriki mashindano hayo mara moja 2015.
Suarez (katikati ) won the gold ball, Messi (kushoto) won the silver ball and Andres Iniesta (kulia) won the bronze
Messi ambae pia alifunga goli la kwanza limemfanya ashike nafasi ya pili orodha ya wafungaji wa muda wote kwa kufunga magoli 5 katika michezo 5 akishiriki mashindano haya mara tatu mwaka 2009,2011 na 2015.
César Delgado wa Monterrey ambae ndie alikuwa kinara katika rekodi ya ufungaji anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na magoli 5 katika michezo 6 akishiriki michuano hiyo mwaka (2011), 2012, na 2013
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni