Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) litamfikisha kwenye Kamati ya Maadlili mapema
Mwakani baada ya sikukuu ya mwaka Mpya 2016, Mkuu wa Mawasiliano wa
klabu ya Yanga, Jerry Muro kutokana na kauli zake za kibaguzi dhidi ya
Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.
Muro
alimshambulia kwa maneno ya kibaguzi Manara wakati akizungumza na
Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika jana makao makuu ya klabu
ya Yanga jijini Dar es Salaam.
Kauli
ya Muro dhidi ya Manara ni kinyume na Katiba ya TFF, Shirikisho la Soka
Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ambao zinapiga
vita vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote katika mpira wa miguu.
Mapema
mwaka huu, Muro alifikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kutokana na
kumshambulia na kumdhalilisha kupitia vyombo vya habari aliyekuwa Kaimu
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Fatma
Abdallah. Kamati ya Nidhamu ilimwadhibu kwa kumpiga faini ya Sh milioni
5.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni