Aliyekuwa meneja wa timu ya taifa ya Uholanzi Guus Hiddink ameteuliwa kuwa kaimu meneja wa Chelsea hadi mwisho wa msimu.
Ameteuliwa baada ya Jose Mourinho kufutwa Alhamisi.
"Nimefurahia
kurejea Stamford Bridge. Chelsea ni moja ya klabu kubwa duniani lakini
haimo pale inakofaa kuwa kwa sasa. Hata hivyo nina uhakika tunaweza
kubadilisha mambo,” amesema Hiddink baada ya kuteuliwa. “Nasubiri kwa
hamu kufanya kazi na wachezaji na wakufunzi wenzangu wapya katika klabu
hii kubwa na kufufua uhusiano wangu mzuri na mashabiki wa Chelsea.”
Hiddink, aliwahi kuinoa Chelsea wakati mmoja, alipowasaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2009, lakini bado hajatia saini mkataba.
The Blues wamo nambari 16 ligini kwa sasa baada ya kushindwa mechi tisa kati ya 16 walizocheza msimu huu Ligi Kuu Uingereza.
Hiddink
alishinda mataji sita ya ligi ya Uholanzi na Kombe la Ulaya akiwa
meneja wa PSV Eindhoven ya Uholanzi katika vipindi viwili.
Pia
aliongoza timu za taifa za Korea Kusini, Australia na Urusi kabla ya
kujiunga na Chelsea mara ya kwanza kujaza pengo lililoachwa na Luiz
Felipe Scolari Februari 2009.
Alijiuzulu
wadhifa wake kama mkufunzi wa timu ya Taifa ya Uholanzi mwezi Juni,
baada ya kutofanya vyema katika juhudi za kuwasaidia kufuzu kwa Euro
2016.
Mwishowe Uholanzi hawakufuzu kwa michuano hiyo.
BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni