TANZANIA imekwea kwa
nafasi tatu kutoka nafasi ya 135 mpaka nafasi ya 132 katika viwango vya
ubora vya soka duniani ambavyo hutolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA lakini imeendelea kuburuza mkia kwa nchi za Afrika
Mashariki.
Uganda bado wameendelea kuwa vinara kwa nchi za Afrika
Mashariki wakishika nafasi ya 13 kwa Afrika na 63 duniani wakifuatiwa na
Kenya wanashika nafasi ya 25 Afrika na 98 duniani huku Rwanda
wakifuatia katika nafasi ya 27 Afrika na 101 Duniani. Burundi ndio
wanafuatia kwa kuwa nafasi ya 33 Afrika na 112 duniani huku Tanzania
wakiburuza mkia kwa kushika nafasi ya 42 kwa Afrika.
Kwa upande wa
Afrika Ivory Coast wameendelea kukaa kileleni kwa nchi za Afrika
wakikwea mpaka nafasi ya nafasi ya 19, wakifuatiwa na Algeria ambao
wameporomoka kwa nafasi mbili mpaka ya 28, Ghana ni wa tatu katika
nafasi ya 33.
Kwa upande wa orodha hizo duniani, Ubelgiji bado
wameendelea kukaa kileleni mwa msimamo wakifuatiwa na Argentina
waliokwea kwa nafasi moja huku Hispania nao wakikwea katika nafasi ya
tatu kuwaondoa Ujerumani ambao wameporomoka mpaka nafasi ya nne na Chile
wamebaki nafasi yao ya tano waliyokuwepo mwezi uliopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni