Cheryshev ambaye alifunga bao la kuongoza katika ushindi mabao
3-1, alikuwa na kadi tatu za njano katika klabu yake ya zamani ya
Villarreal katika michuano hiyo msimu uliopita ambazo zinamfanya kupata
adhabu ya kutocheza mechi moja msimu huu.
Lakini nyota huyo mwenye umri
wa miaka 24 ambaye aliichezea Villarreal kwa mkopo msimu uliopita
amesisitiza hajapata taarifa yeyote kuhusiana na adhabu hiyo.
Klabu ya
Cadiz imethibitisha kuwa wanatarajia kutuma malalamiko yao rasmi
kuhusiana na tukio hilo ambalo linaweza kupelekea Madrid kuondolewa
katika michuano hiyo.
Klabu ya Osasuna walienguliwa katika michuano ya
Kombe la Hispania Septemba mwaka huu baada ya kumtumia mchezaji Unai
Garcia ambaye alikuwa katika adhabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni