MWANARIADHA nyota
mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius amekutwa na hatia ya mauaji
baada ya Mahakama ya Rufani ya nchi hiyo kukubali rufani iliyowasilishwa
na upande wa mashitaka.
Upande wa mashitaka ulitaka Pistorius ahukumiwe
kwa kosa la mauaji badala ya ile hukumu ya awali ya kuua bila kukusudia
aliyopewa.
Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari mwaka
2014 baada ya kumfyatulia risasi mara nne kupitia mlango wa bafuni
uliokuwa umefungwa.
Kwasasa wanariadha huyo alikuwa akitumikia kifungo
cha nje baada ya kukaa jela kwa mwaka mmoja kati ya mitano
aliyohukumiwa. Pistorius sasa atarejea tena mahakamani kwa ajili ya
uamuzi wa hukumu mpya dhidi yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni