KAIMU KAMISHNA WA TRA, DK PHILLIP MPANGO |
Juma lililopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
liliaga timu ya Taifa ya Vijana Chini ya umri wa miaka 15 (U15) ikianza ziara
yake ya Afrika Mashariki kuanzia kucheza na Burundi mjini Kigoma na baadaye
Kigali, Rwanda, Kampala, Uganda na mwisho Nairobi Kenya.
Bahati mbaya ziara hiyo itaishia Mwanza na Kigoma kufuatia
Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala kuzuia fedha kwenye akaunti zote
za Shirikisho kwa madai ya kulipwa kiasi cha Shilingi 1,637,334,000 (bilioni
1.6 tshs) ikiwa ni kodi kwa kipindi cha 2010 – 2013 sehemu kubwa ikiwa ni
makato kwenye mishahara (PAYE) ya walimu wa kigeni, Jan Poulsen, Kim Poulsen na
Jacob Michelsen na vilevile kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo wa
Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Brazil uliofanyika mwaka 2010.
Walimu
wa Timu za Taifa wamekuwa wakilipiwa mishahara na Serikali na hivyo TFF
haikuwajibika kuwakata kodi. Aidha, mchezo kati ya Tanzania na Brazil
ulisimamiwa na kamati maalum ya Serikali na fedha zake hazikuingizwa katika
akaunti za TFF.
Kutokana
na hatua hii ya TRA shughuli nyingine za mpira zitakazohathirika nazo ni:
1.
Kulipia madeni ya usafiri, chakula na posho za Timu za Taifa zilizoshiriki
mtoano wa kombe la Dunia na mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Challenge
Cup)
2.
Program za mpira wa Wanawake na vijana zitalazimika kusimama.
3.
Mashindano ya kombe la Shirikisho raundi ya pili iko kwenye hatihati kwani
hakuna fedha za kugharimia michezo hiyo.
4.
Mashindano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoendelea yatalazimika kusimama
vilevile. Mashindano haya TFF imekuwa ikiyaendesha bila mdhamini.
5.
Vifaa vya michezo (Mipira) kwa ajili ya shule za msingi na vituo vya maendeleo
(Regional Football Development Centres) vinatarajiwa kuwasili nchini wakati
wowote na TFF haitakuwa na uwezo wa kulipia usafirishaji na ushuru wake.
6.
Malipo ya gharama za kambi na karo kwa ajili ya vijana wa timu ya Taifa ya
vijana chini ya miaka 13 walioko shule ya Alliance Academy ya jijini Mwanza.
7.
Huduma za kiutawala ikiwa ni pamoja na utunzaji viwanja na majengo, maji,
umeme, ulinzi pamoja na mishahara na stahiki nyingine za wafanyakazi
8.
Mwelekeo na mwitikio mzuri wa wadhamini uko kwenye hatari ya kupotea pindi
mashindano na shughuli wanazozidhamini zitakapofubaa au kusimama kabisa.
9.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wa Mwaka 2015
uliopangwa kufanyika Tanga 19-20 Desemba 2015 sasa una hatihati ya kuweza
kufanyika.
Hata
hivyo, kwa kutambua umuhimu wa ulipaji kodi na wajibu wa Mamlaka ya Mapato
katika kuhakikisha kodi inakusanywa kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya
Taifa,TFF ipo katika mawasiliano na TRA katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa
suala hili ikiwa ni pamoja na kupitia upya mahesabu ili kujua wajibu halisi
(net liability) wa TFF na namna ya kulipa au kulipwa kutegemea ulali wa
mahesabu.
Hii si
mara ya kwanza hili kujitokeza, lilijitokeza Oktoba 2012 na shilingi
157,407,968 iliyokuwa mgawo wa vilabu kuchukuliwa na TRA. Kufuatia tukio hilo,
yalifanyika mazungumzo kati ya TFF na serikali ambamo ilikubaliwa kwamba fedha
hizo zitarudishwa TFF na mpaka sasa TFF inafuatilia fedha hizo.
Kwa
taarifa hii TFF inaomba utulivu kwa wanamichezo wote pamoja na ushirikiano wa
karibu kutoka katika vyombo vyote husika ikiwemo TRA na wadau wengine ili jambo
hili lipate ufumbuzi wa kudumu utakaoleta tija kwa serikali ya awamu ya tano
ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika maendeleo ya mpira wa miguu na
michezo kwa ujumla wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni