MENEJA wa Arsenal,
Arsene Wenger amebainisha kuwa jambo moja kuwa linalompa nguvu ya
kusonga mbele kwa kipindi kirefu katika shughuli zake za ukocha ni
muziki wa Bob Marley.
Wenger ni shabiki wa kutupwa wa mwanamuzi huyo wa
rege wa Jamaica ambaye kazi zake hupenda kuzisikiliza mara nyingi pindi
akiendesha kuelekea katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
Akihojiwa na
gazeti moja la Ufaransa, Wenger alikiri kumhusudu Bob Marley kwasababu
alikuwa sio mzushi bali mkweli nay eye huwapenda watu wa aina
hiyo.
Arsenal itajitupa uwanjani kesho kukwana na Sunderland katika
mchezo wa Ligi Kuu huku pia wakikabiliwa na mchezo wa kufa na kupona wa
michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Olympiakos jijini Athens
Jumatano ijayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni