BEKI wa Barcelona, Dani
Alves amesisitiza Cristiano Ronaldo hakustahili kuwepo katika orodha ya
mwisho ya wachezaji watatu watakaogombea tuzo ya Ballon d’Or na kudai
kuwa Neymar amekuwa mchezaji wa pili bora duniani baada ya Lionel
Messi.
Wote wawili Messi na neymar wametajwa katika orodha hiyo ya
mwisho sambamba na nyota huyo wa Real Madrid ambaye amefunga mabao 16
katika mechi 18 za mashindano yote alizochez msimu huu.
Pamoja na hayo,
Alves hadhani kama Ronaldo alistahili kuwepo katika kinyang’anyiro hicho
ambacho mshindi wake atajulikana Januari mwakani.
Alves amesema Messi
anaongoza kwasababu ya uwezo wake mchezoni na kwasasa anayemfuatia kwa
ubora ni Neymar.
Beki huyo wa kimataifa wa Brazil aliendelea kudai kuwa
Ronaldo hakustahili kuwepo kabisa katika orodha hiyo kwani haiangalii
suala la ufungaji pekee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni