MSHAMBULIAJI nyota wa
Barcelona, Lionel Messi amefanikiwa kutimiza idadi ya mashabiki milioni
30 wanaomfuata katika mtandao wa kijamii wa Instagram jana na ametumiwa
pongezi na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa timu ya Golden State
Warriors, Stephen Curry.
Kufuatia mafanikio hayo, Messi alituma picha
katika mtandao huo akionyesha fulana ya Barcelona yenye namba 30
mgongoni ambayo aliivaa katika mchezo wa la Liga kwa mara ya kwanza
akiwa na timu hiyo.
Picha hiyo ya Messi ilikwenda sambamba na ujumbe wa
kuwashukuru mashabiki wake hao kwa kumuunga mkono kwa kipindi chote
hicho.
Lakini pamoja na hayo, Messi pia alipongezwa na Curry ambaye
alimualika kwenda kushuhudia moja ya mechi za Golden State Warroirs siku
za mbeleni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni