Kikosi cha Real Madrid cha vijana chini ya miaka 17 kilipoteza mchezo wake katika ligi ambayo hushirikisha vijana chini ya miaka 17 nchini Hispania mbele ya watani wao wa jadi Athletico Madrid.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kusisimua ulishuhudia mtoto wa gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Real Madrid ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi, Luca Zidane ambae ni golikipa wa kikosi cha vijana alimpiga kichwa mchezaji wa Atletico Madrid.
Tukio hilo ambalo liliwashangaza wengi na kukumbuka tukio ambalo alilifanya baba wa Luca,Zinedine Zidane katika kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa timu ya taifa ya Italia,Marco Materrazi kitendo ambacho kilisababisha apewe kadi nyekundu.
Luca amefananishwa na Baba yake kwa kitendo hicho kilicho pelekea kupewa kadi nyekundu na kuacha timu yake kufungwa magoli 4-2.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni