.

Story ya Javier Mascherano na kesi ya ukwepaji kodi imefikia tamati.
Kama ilivyotegemewa, Muargentina huyo sasa itabidi alipe kiasi kikubwa cha faini baada ya kukubali kosa ya kukwepa kodi mwanzoni mwa mwaka.
Mascherano ameamriwa kulipa faini ya €816,000 (£588,000), ambayo ni fedha nyingi sana – ukizingatia mchezaji huyo analipwa £130,000 kabla ya kodi.
Mchezaji huyo pia amehukumia kifungo cha mwaka mmoja jela, lakini kama ilivyo kesi za watu wengi maarufu – Mascherano hatokwenda jela baada ya mawakili wake kufikia makubaliano maalum na mahakama na aaendesha mashtaka.
Tukio hilo limejiri huku Barcelona wakikabiliana na mchezo mgumu kule Mestalla watakapo wafuata Valencia. TAKWIMU MCHEZO WA LEO VALENCIA VS BARCELONA


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni