Mshambuliaji nyoita wa Barcelona, Lionel Messi ameonyesha mapenzi makubwa kwa nyota mwingine wa zamani wa timu hiyo, Ronaldinho.
Messi amechukua jezi yake namba 10 na kuandika ujumbe mzuri wa kuonyesha shukurani kwa Ronaldinho ambaye walicheza wote Barcelona katika timu kubwa kuanzia mwaka 2004 hadi 2008.
Wakati huo
Ronaldinho ndiye alikuwa mchezaji nyota zaidi na Messi ameonyesha kufurahishwa
na namna Mbrazil huyo alivyomuunga mkono wakati akikua kisoka wakati akipanda
timu ya wakubwa akiwa na miaka 16.
Baadaye kupitia
mtandao wa Instagram, Ronaldinho ,36, alionyesha kuwa ameipokea jezi hiyo kama
zawadi bora kabisa kwake. Ronaldinho ndiye aliyemrithisha Messi jezi namba 10.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni