MWAMUZI wa Thailand
ambaye alishambuliwa na mashabiki wenye hasira wa klabu ya ligi daraja
la tatu kufuatia kufungwa, amefungiwa miezi sita kutokana na uchezeshaji
mbaya katika mchezo huo.
Mwamuzi huyo Pichit Thongchanmoon alivamiwa na
mashabiki wa timu ya Satun United kufuatia kufungwa bao bao 1-0
nyumbani na Khoh Kaen United Novemba 22 mwaka huu.
Satun walifungiwa
miaka mitatu wiki iliyopita kwa tukio hilo lakini kamati ya Chama cha
Soka cha Thailand imesema Pichit alifanya makosa kadhaa katika mchezo
huo na kumlima adhabu hiyo.
Kamati hiyo imesema Pichit alitakiwa kuipa
Satun penati na kuwa mwamuzi huyo alikuwa mbali na eneo husika mara
nyingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni