RAIS ABDEL AZIZ
Rais wa Mauritania, Mohamed
Ould Abdel Aziz ametoa kali ya mwaka baada ya kulazimisha mechi iishe katika
dakika ya 63 na kutaka timu zipigiane
mikwaju ya penalti.
|
Rais huyo alionekana kukerwa
na uchezaji wa taratibu katika mechi ya Super Cup iliyokuwa inazikutanisha timu
za FC Teyragh-Zeina na ACS Ksar na tayari zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Mwamuzi alifikishiwa ujumbe
huo ambao ulitoka kwa rais aliyekuwa jukwaani. Naye hakuwa na ujanja zaidi ya
kutimiza hilo, mikwaju ya penalti ikapigwa.
Hata hivyo, suala hilo
lilikuwa gumzo na kusababisha tafrani baadhi ya mashabiki wa soka wa Mauritania
wakilaani uamuzi huo wa rais wa nchi yao kuingilia masuala ya soka.
Baada ya hapo, Ikulu ya Mauritania ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikikanusha rais huyo kuhusika na suala hilo huku ikisisitiza ni uzushi mtupu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni