Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo, usiku wa December 8 katika mchezo dhidi ya Malmoe FF
wa kuhitimisha mechi za Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alivunja
rekodi yake mwenyewe aliyoiweka msimu uliyopita, kabla ya mchezo huo
uliyomalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 8-0, Ronaldo
alikuwa anashikilia rekodi ya kuongoza kwa kufunga magoli mengi katika
mechi za Makundi, kwani alifunga magoli 9 msimu uliyopita.
Usiku wa December 8 aliingia uwanjani
akiwa tayari kafunga jumla ya magoli 7 katika mechi 5 zilizopita za
hatua ya makundi, hivyo kufunga kwake goli nne katika mchezo dhidi ya Malmoe FF
kulimfanya afikishe jumla ya magoli 11 na kuvunja rekodi yake ya msimu
uliyopita, rekodi ambayo hakuna mchezaji aliyekuwa kaifikia. Mtu wangu
wa nguvu hiyo sio rekodi ya kwanza ya Ronaldo, naomba nikusogezee rekodi 10 kali za Ronaldo.
1- Wakati akicheza Man United Ronaldo alifanikiwa kuvunja rekodi ya mkongwe wa timu hiyo George Best ya ufungaji wa magoli 33 katika msimu wa 1967/1968 na kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza wa Ureno kucheza kwa mafanikio Man United.
2- Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi kubwa za Ulaya kufunga magoli 50 na zaidi katika msimu mmoja. rekodi ambayo aliiweka kwa kufunga magoli katika mashindano matano tofauti.
3- Staa huyo pia anashikilia rekodi ya
kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 100 ya Ligi katika kipindi
kifupia, kitendo ambacho kimemfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufanya hivyo, Hata hivyo magoli hayo yalimfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza wa Laliga kuzifunga timu zote 19 za Laliga zilizocheza dhidi ya Real Madrid.
4- Ronaldo
anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 17 katika
msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifanya hivyo katika msimu wa
2013/2014.
5- Ronaldo
aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli 200 za haraka za
Laliga katika jumla ya michezo 178 December 2014. Alifunga hat-trick
dhidi ya Celta Vigo na kufikisha jumla ya hat-trick 23 zilizoingia katika rekodi ya Laliga.
6- Ronaldo
alifunga jumla ya hat-trick 8 katika msimu mmoja wa 2014/2015 na kuweka
rekodo ya kufunga hat-trick nyingi zaidi kuwahi kufungwa katika msimu
mmoja wa Ligi.
7- Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Sporting Lisbon kucheza katika vikosi vya (U-16), (U-17), (U-18), timu B na kikosi cha kwanza cha kwanza cha Sporting Lisbon yote hiyo amecheza katika msimu mmoja.
8- Wakati anacheza Man United Ronaldo
aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu wa Ligi Kuu Uingereza kushinda
tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mara mbili mfululizo, alifanya hivyo
mwaka 2006 kwa kutwaa tuzo hiyo mwezi November na December. Wengine
waliowahi kufanya hivyo ni Robbie Fowler mwaka 1996 na Dennis Bergkamp mwaka 1997.
9- Ronaldo ni mchezaji wa pili kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mara nyingi, ametwaa mara tatu mwaka 2008, 2013 na 2014, anayeongoza kwa rekodi hiyo ni Lionel Messi aliyetwaa mara nne.
10- Ronaldo ndio mchezaji wa kwanza Ligi Kuu Uingereza kuwahi kutwaa tuzo nne za PFA na FWA kwa msimu mmoja, Ronaldo alifanya hivyo mwaka 2007 akiwa katika klabu ya Man United.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni