Lionel Messi ni staa wa soka wa kimataifa wa Argentina ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania aliyojiunga nayo mwaka 2001 na mwaka 2003 akaanza kuichezea FC Barcelona C.
Lionel Messi anatajwa kuwa ni moja kati ya wachezaji soka wenye rekodi za kusisimua zaidi duniani.
Hizi ni rekodi 5 za kusisimua za Lionel Messi stori kutoka sokkaa.com
5- Lionel Messi sio tu anatajwa kuwa mchezaji bora wa Dunia, ila wachambuzi wa masuala ya soka wanamuita ni moja kati ya wachezaji bora wa soka waliowahi kutokea katika historia ya soka. Messi ndio mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or mara 4, kwani hakuna mwingine aliyewahi kufanya hivyo.
4- Mwaka 2012 Lionel Messi alifanikiwa kuvunja rekodi ya Muller ambaye alikuwa amefunga jumla ya goli 85 kwa mwaka, rekodi ambayo ilidumu toka mwaka 1972 ila Lionel Messi
mwaka 2012 amevunja rekodi hiyo kwa kufunga jumla ya magoli 91 katika
mechi za mashidano yote na kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka 40 bila
kuvunjwa.
3- Staa huyo wa Argentina
ndio mchezaji pekee mwenye rekodi ya kufunga magoli katika mechi 21
mfululizo za Ligi Kuu, rekodi ambayo aliiweka msimu wa 2012/2013.
2- Ni mchezaji wa kwanza kuzifunga mfululizo timu zote za Ligi Kuu, msimu wa 2012/2013 Lionel Messi alifanikiwa kuzifunga mfululizo timu zote 19 pinzani katika Ligi Kuu Hispania, licha ya kuwa Cristiano Ronaldo amewahi kufanya hivyo msimu wa mwaka 2011/2012 ila Lionel Messi amefunga mfululizo yaani kwa kufuatana.
1- Lionel Messi ndio mchezaji pekee aliyewahi kutwaa mara mbili tuzo ya golden ball ya michuano ya klabu Bingwa Dunia ambayo mwaka huu inafanyika Japan, rekodi ambayo aliiweka mwaka 2009 na 2011.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni