Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefanya balaa kwenye usiku wa Ulaya baada ya kupasia nyavu mara nne wakati klabu yake ikiifanyia mauaji klabu ya Malmoe FF kwa kuipa kibano cha magoli 8-0 kikiwa ni kipigo kikubwa kwa michezo ya UEFA Champions League iliyopigwa December 8, 2015.
Benzema alianza kupiga goli mbili za mapema dakika ya 12 na 24 wakati Ronaldo yeye akichungulia nyavu dakika ya 39 kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilizidi kuwa kibaya kwa upande wa Malmoe kwani walijikuta wakiruhusu magoli matano ndani ya kipindi hicho.
Cristiano Ronaldo alipiga bao tatu ndani ya kipindi cha pili wakati Benzema na yeye akikamilisha hat-trick yake kwa kupiga bao la dakika ya 79 huku Kovacic akifunga bao moja kukamilisha ushindi wa magoli 8-0.
Ronaldo amweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 11 kwenye michuano ya UEFA Champions League kwenye hatua ya makundi lakini pia kufunga hat-trik ndani ya dakika 11 za kipindi cha pili na amekuwa mchezaji wan ne kwenye klabu yake kufunga magoli manne kwenye mchezo wa UEFA Champions League.
Cristiano Ronaldo na Kareem Benzema ni washambuliaji wawili waliofunga jumla ya magoli saba kwenye mchezo huo huku lika mmoja akiwa amefunga hat-trick lakini Ronaldo yeye akaongeza bao moja zaidi ya Benzema.
Ushindi huo umeipa Madrid nafasi ya kuongoza kundi A ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 16 baada kucheza michezo 6 ikifuatiwa na PSG yenye pointi 13 baada ya kushuka dimbani mara 6 pia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni