Vilabu vya Simba, Azam, Yanga na Mtibwa Sugar vinatarajiwa kushiriki katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi yatakayoanza kutimua vumbi Januari Mosi hadi 14, mmwezi ujao visiwani Zanzibar.
Timu hizo zimeteuliwa kushiriki michuano hio na chama cha kandanda visiwani Zanzibar, ZFA na kupata baraka za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Katibu Mkuu wa chama cha kandanda Zanzibar (ZFA) Khasim Salum, amesema kuna uwezekano mdogo wa kualika timu za nje ya nchi na kuongezea kuwa hadi sasa maandalizi yamefikia hatua nzuri.
Simba ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi baada ya kumfunga Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penati.
Ushiriki wa Azam, Simba , Mtibwa na Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi unamaanisha Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara itasimama hadi tarehe 16 mwezi wa kwanza, jambo ambalo lilianishwa kwenye ratiba iliyotolewa na TFF.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni