Michuano ya klabu Bingwa Dunia ilianza December 10 2015 katika ardhi ya Japan, hii ni michuano ambayo inatafuta Bingwa wa Dunia kwa ngazi ya vilabu, kwa upande wa bara la Afrika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio ilikuwa inawakilisha bara hili.
TP Mazembe ambayo inachezewa na watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ilianza kucheza michuano hiyo December 13 katika hatua ya robo fainali dhidi ya klabu ya Sanfrecce na kukubali kipigo cha goli 3-0, huu ni mchezo ambao watanzania wengi walikuwa wanautazama, kwani Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kushiriki michuano hiyo.
Sanfrecce walianza kupata goli la kwanza dakika ya 44 kupitia kwa Shiotani ikiwa ni dakika moja imesalia kabla ya kwenda mapumziko. TP Mazembe walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha ila dakika ya 56 kipindi cha pili Chiba akapachika goli la pili kwa Sanfrecce, licha ya TP Mazembe kutokata tamaa, goli la dakika ya 78 la Asano ndio lilihitimisha safari ya TP Mazembe kwenda hatua ya nusu fainali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni