STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 5 Desemba 2015

UGANDA MABINGWA WAPYA CHALLENGE 2015, WAICHAPA RWANDA 1-0

UGANDA wamefanikiwa kutwaa taji la 14 la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuifunga Rwanda bao 1-0 jioni ya leo nchini Ethiopia katika mchezo wa fainali.
 
Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Ceasar Okhuti aliyemalizia kwa kichwa krosi ya Dennis Okot kwa kumtungua Eric Ndayishimiye dakika ya 15.
 
Kocha Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic ambaye amewahi kuifundisha Rwanda alikuwa mwenye furaha na akasema Uganda imedhihirisha ubora wake katika ukanda wa CECAFA.

“NInafurahia kazi, ni furaha kubwa, tumedhihirisha sisi ni bora katika ukanda huu, tukiwa timu pekee iliyofuzu hatua ya makundi kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 Urusi, na tunabeba Kombe la Challenge,”amesema.
 
Mapema katika mchezo uliotangulia, wenyeji Ethiopia walimaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga Sudan kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1.
 
Kikosi cha Uganda kilikuwa; Ismail Watenga, Denis Okot, Joseph Ochyaya, Juuko Murushid, Richard Kassaga, Muwanga Bernard, Ivan Ntege, Erisa Sekisambu,Mutyaba Muzamir, MIya Faruku na Ceasar Okhuti.
 
Rwanda: Eric Ndayishimiye, Michel Rusheshangonga, Jacques Tuyisenge, Celestin Ndayishimiye, Abdul Rwatubyaye, Faustin Usengimana, Haruna Niyonzima, Yannick Mukunzi, Dominique Savio Nshuti, Jean-Baptiste Mugiraneza na Jean-Claude Iranzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox