MENEJA wa Bayern Munich,
Pep Guardiola amekanusha tetesi kuwa anaweza kujiunga na Real Madrid
kama akiondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi mwakani.
Mkataba wa
miaka mitatu wa Guardiola kwa mabingwa hao wa Ujerumani unatarajiwa
kumalizika mwishoni mwa msimu huu na klabu hiyo inatarajiwa kutangaza
uamuzi wake kama ataendelea kubakia huko.
Kocha huyo wa zamani wa
Barcelona amekuwa akihusishwa kwa karibu na tetesi kwenda Ligi Kuu huku
Manchester City na Manchester United zikitajwa kumuwania.
Lakini taarifa
zilizotolea hivi karibuni na vyombo vya habari vya Hispania zimedai
kuwa Madrid imetuma watu wake kuona kama Guardiola atapenda kutua
Santiago Bernabeu.
Akiulizwa kuhusu suala hilo, Guardiola alikanusha na
kuongeza kuwa hadhani kama anaweza kuendana na klabu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni