Alexandre Tato amesema anafuraha kujiunga na Chelsea baada ya mshambuliaji huyo wa Brazil kuwasili jijini London kukamilisha uhamisho wake wa mkopo.
Wakati ikiwa bado klabu ya Chelsea haijasema chochote juu ya uhamisho wa nyota huyo kutoka Corinthians na kutua Stamford Bridge yeye tayari amesema “Chelsea ni makazi yake mapya”.
Kutua kwa Pato jijini London kumeifanya Chelsea itangaze kuuzwa kwa kiungo wake Ramires ambaye amejiunga na klabu ya Jiangsu Suning ya China.
Pato ameiambia Sky Spors: “Ninafuraha. Nipo hapa kutokana na ndoto zangu. Hapa ni makazi yangu mapya. Asante Chelsea kwa sapoti
, asante kwa mashabiki wangu kwa support kupitia Instagram, Twitter na Facebook”.
“Ninahitaji kucheza. Sijui hata cha kusema kwasababu ninafuraha. Ninahamu ya kucheza na kufahamiana na marafiki zangu wapya kwenye timu. Ninahitaji sana kuichezea Chelsea”.
Pato ambaye ameichezea Brazil michezo 27, hajacheza mchezo wowote tangu November mwaka uliopita, anatarajiwa kufanyiwa vipimo kabla ya kusaini mkataba wa kujiunga na wakali hao wa Stamford Bridge.
ALEXANDRE PATO CAREER STATS
Internacional 2006-2007
12 goals in 27 games (in all competitions)
AC Milan 2007-2013
63 goals in 150 games
Corinthians 2013-2014
17 goals in 62 games
Sao Paulo (loan) 2014-2015
38 goals in 95 games
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni