STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 28 Januari 2016

SABABU 5 ZINAZOWEZA KUIFANYA LEICESTER CITY KUCHUKUA UBINGWA EPL MSIMU HUU

 
1. Wana Mwamko, Ari na Kasi
Dharau wapinzani wako, chukulia kila mechi sawa na nyingine, kubwa na ndogo. Cheza kwa kasi thabiti na kwa nguvu ili ufikie malengo.
Leicester walikuwa na pointi 19 baada ya mechi 10 msimu huu, 39 baada ya mechi 19 na Claudio Ranieri amedhamiria kuwapa motisha wachezaji wake. Iwapo Mbweha hao watashinda mechi zote 15 zilizosalia kwa hakika watakuwa mabingwa msimu huu.

2. Takwimu zinawabeba
Hii ni kwa sababu kasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi imekuwa ndogo kwa muda wa miaka 17. Tangu mwanzo wa karne mpya, wastani wa pointi 87.5 umekuwa ukihitajika kwa timu kuwa bingwa.
Kama inavyoonekana, Arsenal na Manchester City zina wastani wa 73.
Kila timu inaweza kuongeza juhudi kupata ubingwa lakini kama ilivyoelezwa hapo juu Leicester haipaswi kuhofu. Wanaweza kudhibiti timu zinazodhibitika, kwa kujiaminisha kuwa timu hizo mbili kubwa hazitafanya chochote.
Kiwango cha kasi ya kushinda taji ni wastani wa pointi 2.3 kwa kila mchezo lakini hata kama Arsenal au Man City watapanda kutoka wastani wao wa pointi 1.91 kufikia kiwango kinachohitajika katika mechi 15 zilizobaki, watamaliza wakiwa na pointi 79 tu - ambazo ni sawa na zile inazolenga Leicester.

3. Michezo ya Akili? Michezo ya akili ni nini? - "Mind Games"
Leicester ni timu ambayo haijisumbui kucheza soka la kuvutia, zaidi wanaangalia ushindi kuliko chochote.
Swali la msingi kuhusu mbinu zinazotumiwa na Arsene Wenger na Manuel Pellegrini. Wote wanaelekeza macho kwenye soka la kuvutia na kumiliki mpira kuliko matokeo. Hii ni mara ya kwanza tangu 1981 (Aston Villa walipoipiku Ipswich katika mechi ya mwisho ya msimu kwa pointi mbili na kushinda ubingwa) mbio za ubingwa kuongozwa na timu inayotumia msuli na inayolenga matokeo.
Wenger na Pellegrini hawatumii ujanja ujanja kushinda mechi.
Leicester City imepona kukutana na makocha kama Alex Ferguson na Jose Mourinho, na kwa sababu hii wataendelea kusonga bila kupata msuko suko wowote. Wasumbufu hawapo.

4. Wasifu wa Ranieri unaongoza njia ya Ubingwa
Kwa mujibu wa Myers-Briggs Type Indicator wasifu wa Ranieri ni ESFP - Mtaalamu mwenye umahiri wa hali ya juu ambaye anapenda mabadiliko katika mazingira yanayomzunguka, hali kadhalika mwenye mtazamo chanya na mtendaji. Kwa ufupi anaweza kushughulika na changamoto zote zinazoweza kuikabili Leicester.

5. Matukio yasiyo ya kawaida, Matokeo yasiyo ya kawaida
Wachambuzi walio wengi hawawapi Mbweha nafasi - ila asilimia 9-13 kwa makisio. Lakini kwa jumla takwimu hizo zimebatilishwa na hali ya Leicester kwa sasa, hazina uhalisia wa matarajio ya awali. Leicester imefanya mambo yasiyo ya kawaida kupata matokeo yasiyo ya kawaida wakati ikiwa ni timu ndogo isiyodhaniwa kufanya chochote.

Fursa ya kucheza Ligi ya Mabingwa inakaribia zaidi kwa hakika, Mbweha ni dhahiri hawawezi kurudi nyuma sasa kwani si jambo rahisi sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox