MSHAMBULIAJI nyota wa
Barcelona, Lionel Messi ameonekana kutokuwa na majeruhi yeyote baada ya
kulazimika kutolewa katika muda wa mapumziko katika mchezo wa La Liga
dhidi ya Athletic Bilbao.
Baada ya kufunga bao la kuongoza katika
ushindi wa mabao 6-0 waliopata jana katika Uwanja wa Camp Nou, nyota
huyo wa kimataifa wa Argentina alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na
Arda Turan baada ya kulalamika kusikia maumivu katika mguu wake wa
kulia.
Ilikuwa ikihofiwa kuwa mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or
alikuwa amepata majeruhi ambayo yangemuweka nje kwa wiki kadhaa. Hata
hivyo, baada ya kufanyiwa vipimo klabu hiyo ilithibitisha kuwa tatizo la
nyota huyo mwenye umri wa miaka halikuwa kubwa kama
ilivyofikiriwa.
Lakini pamoja na hayo haina uhakika kama Messi atakuwepo
katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Mfalme
keshokutwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni