KATIKA
hali inayoashiria ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuelekea kuvurugika , Yanga SC imesema itaondoka nchini Ijumaa kwenda Afrika Kusini
kuweka kambi ya kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga
SC inataka kuondoka nchini siku moja kabla ya mchezo wake wa Ligi Kuu
dhidi ya Coastal Union ya Tanga uliopangwa kufanyika Jumamosi Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga.
Mkuu
wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amesema kwamba kikosi cha timu yao kiinakwenda
Afrika Kusini ili kuhakikisha wanapata maandalizi mazuri kabla ya kuanza
kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi ujao.
Muro
amesema Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Deusdedit Baraka atawasilisha barua
ya kuomba kusogezwa kwa michezo yao kadhaa ili waweze kwenda Afrika
Kusini.
"Ni
kweli Ijumaa tunakwenda Afrika Kusini kwa maandalizi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika na kama ambavyo inafahamika tutaanzia ugenini na Cercle de Joachim Februari 13, mwaka huu, ni hivi karibuni tu,”amesema Muro.
Hatua
ya Yanga inakuja baada ya mechi mbili za Ligi Kuu za Azam FC dhidi ya
Prisons uliokuwa ufanyike Uwanja wa Sokoine, Mbeya Jumamosi wiki hii na
dhidi ya Stand United uliopangwa kufanyika Februari 3, mwaka huu Uwanja
wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kufutwa ili timu hiyo iende Azam
FC Zambia.
Azam FC inatarajiwa kuondoka usiku wa leo kwenda Zambia kushiriki michuano maalum na inatarajiwa kurejea Februari 4, mwaka huu
Mtendaji
Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema leo
kwamba wamepata ruhusa maalum kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
juu ya ziara yao na mechi zao hizo mbili za Ligi Kuu zitapangiwa tarehe
nyingine.
Kawemba
amesema kwamba watakaporejea Februari 4, wataendelea na ratiba
watakayoikuta ya Ligi Kuu, kuanzia mchezo na Mwadui FC Februari 7,
Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Na
Kawemba ameema mechi zao za viporo zitachomekwa katikati ya ratiba yao
kuanzia hapo kulingana na nafasi ambayo itaonekana inafaa kwao na kwa
wapinzani wao.
Azam
FC imealikwa nchini Zambia kushiriki michuano maalumu inayoshirikisha
timu nne, iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa klabu mbili za huko, Zesco
United na Zanaco FC.
Michuano
hiyo itaanza keshokutwa Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola na mbali
na Azam FC, Zesco na Zanaco, timu nyingine itakayoshirki mabingwa wa
Ligi Kuu Zimbabwe, Chicken Inn.
Pamoja
na Azam FC kuruhusiwa kwenda Zambia, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
inatarajiwa kuendelea Jumamosi, Coastal Union wakiikaribisha Yanga SC
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Simba SC wakiwa wenyeji wa African Sports
wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
nyingine ni kati ya JKT Ruvu na Majimaji Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam, Mtibwa Sugar na Stand United Uwanja wa Manungu, Turiani,
Morogoro, Mwadui FC na Toto Africans Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga
na Kagera Sugar dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mwinyi, Tabora.
Jumapili kutakuwa na mchezo mmoja tu, kati ya Mgambo JKT na Ndanda FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Chanzo Bin Zubeir
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatatu, 25 Januari 2016
YANGA NA AZAM KUPANGUA TENA RATIBA YA LIGI KUU (VPL)
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
asante sana kwa taarifa
JibuFuta