Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga SC
wamerejea kileleni mwa ligi kuu ya vodacom baada ya leo kuibuka na ushindi wa
goli 5 -0 mbele ya Majimaji huku Amisi Tambwe akifunga magoli 3.
Katika mchezo wa leo Yanga SC waliuwanza mchezo kwa kasi na kusaka goli la mapema ambapo katika dakika ya 5 kupitia kwa Thaban Kamusoko akitumia vyema pasi ya Deusi Kaseke na kuiandikia yanga goli la kuongoza.
Katika mchezo wa leo Yanga SC waliuwanza mchezo kwa kasi na kusaka goli la mapema ambapo katika dakika ya 5 kupitia kwa Thaban Kamusoko akitumia vyema pasi ya Deusi Kaseke na kuiandikia yanga goli la kuongoza.
Kuingia kwa goli hilo kuliongeza umakini katika safu
ya Majimaji na kupelekea Yanga SC kutengeneza nafasi chache katika kipindi
chote cha kwanza na kupelekea timu kwenda mapumziko yanga sc wakiwa mbele kwa
goli 1-0.
Katika kipindi cha Majimaji FC ambao walifika langoni mwa yanga mara tatu katika kipindi cha kwanza walijikuta wanaruhusu goli la pili katika dakika ya 47 kupitia kwa Donald Ngoma.
Katika kipindi cha Majimaji FC ambao walifika langoni mwa yanga mara tatu katika kipindi cha kwanza walijikuta wanaruhusu goli la pili katika dakika ya 47 kupitia kwa Donald Ngoma.
Msimamo wa Ligi Kuu Msimu Huu
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | YANGA | 15 | 12 | 3 | 0 | 36 | 5 | 31 | 39 |
2 | Azam FC | 15 | 12 | 3 | 0 | 30 | 10 | 20 | 39 |
3 | SIMBA SC | 15 | 10 | 3 | 2 | 23 | 9 | 14 | 33 |
4 | MTIBWA SUGAR | 15 | 8 | 4 | 3 | 17 | 9 | 8 | 28 |
5 | STAND UNITED | 15 | 9 | 1 | 5 | 17 | 12 | 5 | 28 |
6 | T. PRISONS | 15 | 8 | 3 | 4 | 16 | 15 | 1 | 27 |
7 | MWADUI FC | 15 | 7 | 4 | 4 | 18 | 14 | 4 | 25 |
8 | TOTO AFRICANS | 15 | 4 | 5 | 6 | 13 | 18 | -5 | 17 |
9 | MGAMBO SHOOTING | 15 | 4 | 4 | 7 | 13 | 16 | -3 | 16 |
10 | MBEYA CITY | 15 | 3 | 5 | 7 | 13 | 19 | -6 | 14 |
11 | NDANDA FC | 15 | 2 | 6 | 7 | 13 | 17 | -4 | 12 |
12 | JKT RUVU | 15 | 3 | 3 | 9 | 16 | 23 | -7 | 12 |
13 | MAJIMAJI FC | 15 | 3 | 3 | 9 | 9 | 29 | -20 | 12 |
14 | Coastal Union | 15 | 1 | 7 | 7 | 9 | 17 | -8 | 10 |
15 | AFRICAN SPORT | 15 | 2 | 3 | 10 | 4 | 15 | -11 | 9 |
16 | KAGERA SUGAR | 15 | 2 | 3 | 10 | 5 | 19 | -14 | 9 |
Kuingia kwa goli hilo kuliwatoa Majimaji katika mtililiko wao wa kucheza soka na kutaka kwenda mbele kusaka goli la kukomboa ambao walipoteza nafasi mbili za kujipatia goli.
Amisi Tambwe aliiandikia Yanga goli la tatu katika dakika 57 kabla ya kufanya hivyo katika dakika ya 71 na katika dakika ya 84 na kuipatia yanga sc ushindi wa goli 5-0.
Kwa matokeo hayo Yanga wamerejea kilelni baada ya jana Azam FC kuwashusha, huku wakiongeza wigo wa tofauti ya magoli baina yao na Azam FC ambao wana lingana kwa pointi wote wakifikisha pointi 39.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mwadui FC imeshinda
2-1 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na African Sports
imelazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratias Munishi
‘Dida’, Juma Abdul/Said Juma dk22, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Vincent Bossou,
Salum Telela, Simon Msuva/Issoufou Boubacar dk67, Thabani Kamusoko, Donald
Ngoma/Paul Nonga dk78, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
Majimaji: David Burhani, Alex Kondo, Bahati Yusuph, Mpoki Mwakinyuke, Sadiq Gawaza, Lulanga Mapunda/Kennedy Kipepe dk33, Peter Mapunda/Hassan Hamisi dk63, Paul Maona/Godfrey Taita dk70, Marcel Bonaventura, Sixmund Mwakasega na Frank Sekule.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni