STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 24 Februari 2016

JE! UNAFAHAMU KUWA KAMUSOKO ALIWABEBA YANGA,JUUKO SIMBA...............

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/10/vpl2.jpg

MWISHONI mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kulikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara uliozikutanisha Yanga na Simba.

Mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka hapa nchini na ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Ushindi huo umeifanya Yanga kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 46.

Mbali na matokeo ya mchezo huo, kwa upande mwingine timu zote ziliweza kuwatumia wachezaji wao wa kimataifa kwa nafasi walizoamini ndizo wanastahili kucheza, na wale walioonekana hawawezi, wakaishia benchi.

Kwa upande wa Yanga ambayo ina jumla ya profesheno saba sawa na Simba huku Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiweka sheria kwamba kila timu iwe na profesheno wasiozidi idadi hiyo, Wanajangwani hao waliweza kuwatumia sita na mmoja kuishia benchi.

Profesheno wa Yanga waliocheza ni Vincent Bossou (Togo), Amissi Tambwe (Burundi), Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima (wote raia wa Rwanda), Thabani Kamusoko na Donald Ngoma ambao ni Wazimbabwe, huku Issoufou Boubacar raia wa Niger akiishia benchi.

Simba yenyewe iliwatumia watano ambao ni Vincent Angban raia wa Ivory Coast, Justice Majabvi (Zimbabwe), Juuko Murshid, Hamisi Kiiza na Brian Majwega aliyetokea benchi, hawa wote ni raia wa Uganda. Mrundi, Emery Nimubona aliishia benchi huku Mkenya Paul Kiongera akikosekana kabisa kutokana na kuwa majeruhi.

Makala haya inakuchambulia uwezo waaliouonyesha maprofesheno katika mechi hiyo kubwa Afrika Mashariki.



                           

                             YANGA

Twite

Anao uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani ndiyo maana kocha wake, Mholanzi, Hans van Der Pluijm aliamua kumchezesha namba nne kuziba pengo la Kelvin Yondani ambaye alikuwa akimalizia adhabu yake ya kadi nyekundu.

Twite alikuwa akisawazisha makosa kadhaa ya mwenzake, Bossou, na kufanikiwa kujenga ukuta mgumu kwa Yanga.





Bossou

Alichezeshwa ili kuziba pengo la Cannavaro. Alijitahidi kwa uwezo wake na kufanikiwa kumdhibiti kisawasawa Hamisi Kiiza na hata alipoingia Danny Lyanga, hali haikuwa tofauti sana licha ya kupata shida kidogo kumkaba kutokana na usumbufu aliokuwa akiuonyesha Lyanga. Alicheza vizuri, anatakiwa aongeze spidi kwani kuna hatari inaweza kutokea siku akikutana na straika mwenye nguvu na mbio.



Kamusoko

Alikamata kwa kiasi kikubwa kiungo cha kati na kutengeneza mashambulizi kwa wapinzani. Alikuwa akipambana na Mwinyi Kazimoto pamoja na Jonas Mkude, hakuna asiyemjua Kamusoko, kila siku zinavyozidi kwenda ubora wake unadhihirika. Alikuwa chachu kubwa ya Yanga kupata pointi tatu. Kwa upande wa huyu ndiye nyota wa mchezo.



Niyonzima


Alicheza kama winga na wakati mwingine alikuwa akiingia kati kusaidia kutafuta mipira na kuisambaza. Alicheza vizuri kwa dakika 52 kabla ya kutolewa na kuingia Simon Msuva.

Bado hajarudi katika kiwango kile cha zamani, na mashabiki wa Yanga wamekuwa wakimlalamikia mara kwa mara kwamba hucheza chini ya kiwango dhidi ya Simba pekee, lakini juzi alijitahidi.



Tambwe

Kwa mara nyingine anawafunga Simba msimu huu, katika mechi ya kwanza ambayo Yanga ilishinda 2-0, Tambwe alifunga bao moja huku lingine likifungwa na Malimi Busungu.

Ujanja wake na kutumia nguvu ya kupambana na mabeki, alifanikiwa kumsumbua Juuko Murshidi ambaye anasifika kwa kucheza kwa umakini na nguvu.



Ngoma

Aliivuruga safu ya ulinzi ya Simba vilivyo. Ndiye aliyesababisha beki wa Simba, Abdi Banda atolewe uwanjani kwa kadi nyekundu baada ya kuonekana beki huyo ameshindwa kumkaba Ngoma na kumchezea rafu mbili zilizofanana ndani ya dakika tatu.

Anapambana, ana kasi, kutokana na safu ya ushambuliaji ya Yanga ilivyo kwa sasa, siku akikosekana yeye na Tambwe, ni wazi timu hiyo itapata shida kwenye kusaka ushindi.



                              SIMBA

Angban

Siku zote huwa mtulivu awapo uwanjani ndiyo maana mpaka sasa amefanikiwa kudaka takribani mechi 16 za ligi mfululizo na kumuacha Peter Manyika akiishia benchi.

Katika mchezo huu kwake ulikuwa ni wa kwanza dhidi ya Yanga na alifanya kosa moja tu ambalo lilitumiwa na Tambwe kufunga bao la pili, lakini alijitahidi vilivyo kuuwahi mpira aliorudishiwa na beki wake, Hassan Kessy, lakini alichelewa kufika na kumpa fursa Ngoma afunge bao la kwanza. Ataendelea kuwa msaada kwa Simba katika kipindi hiki.



Juuko

Ndiye aliyecheza vizuri zaidi kwa dakika zote kwa upande wa Simba. Alipambana vilivyo na washambuliaji wa Yanga kwa nyakati tofauti huku akikosa msaada wa uhakika.

Dakika ya 72 alichelewa kidogo tu kumkaba Tambwe, wakafungwa. Lakini hiyo haiwezi kumfanya asiwe bora katika mchezo huu.



Majabvi

AWALI tuliaminishwa kuwa Mzimbabwe huyu anazimudu nafasi mbili uwanjani, kiungo mkabaji na beki wa kati. Hakukuwa na ubishi kutokana na kumuona katika mechi kadhaa za ligi akicheza vizuri katika nafasi hizo zote kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Wapo wachezaji wengi ambao ukimchezesha namba tofauti na ile tuliyozoea kumuona hakutakuwa na tofauti, lakini kwa Majabvi huko nyuma alicheza vizuri sijui labda kutokana na aina ya timu alizokutana nazo kwani mbele ya Yanga alionekana kuwa ‘nyanya’.

Kocha wa Simba Jackson Mayanja alimchezesha Majabvi beki wa kati baada ya Abdi Banda kutolewa kwa kadi nyekundu. Bao la kwanza la Yanga lilitokana na makosa ya Hassan Kessy kurudisha kwa kipa wake mpira mfupi, lakini ukiangalia vizuri Majabvi hakuwa sehemu sahihi ya kutoa msaada.



Kiiza

Haikuwa siku nzuri kwake kwani kwa dakika 59 alizocheza na kumpisha Danny Lyanga, alifanikiwa kupiga shuti moja lililodakwa na kipa wa Yanga, Ally Mustafa ‘Barthez’. Hii imetokana na kukosa usaidizi sahihi kutoka kwa Ibrahim Ajib, lakini pia umakini wa mabeki wa Yanga, Bossou na Twite ulimfanya Kiiza ‘azurure’ uwanjani muda mwingi.



Majwega

Bado ana nafasi ya kujiuliza ni kwa nini huwa haanzi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza. Alitumia dakika 15 tu kwenye mchezo huu, aliingia uwanjani dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Ajib, hakuweza kubadilisha chochote mpaka mwisho wa mchezo.



www.mdosejr@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox