Marehemu enzi za uhai wake
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa staili yake ya kuimba kama mlevi, Joni Woka amefariki dunia .
Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa Joni Woka amefariki katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.
Joni Woka alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa garage maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani.
Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.
Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za walimu, Bitozi, Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.
R.I.P JONI WOKA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni