Mkataba wa kazi huwa ni siri kubwa kati ya pande mbili ambazo zinafanya kazi pamoja.
Sasa kuna mkataba umevuja ambao unamhusu Cristiano Ronaldo na kampuni ya MIM ambayo ni agency ya kampuni ya kutoa huduma ya internet inaitwa Mobily huko Saudi Arabia.
Kazi hii ilifanyika mwaka 2012 na mkataba huo ulikua na vipengele vya msingi vifuatavyo.
Cristiano Ronaldo alitakiwa ku-sign jezi 5 za Portugal kwa ajili shindano la wateja wa Mobily, aweke post mara mbili aki-mention Mobily kuzungumzia hiyo huduma mpya ya 4G kwenye page za Faceboo na Twitter, kufanya photo shooting na video recording chini ya masaa 4:30.
Picha hizo zitatumika kwenye promotion isiyozidi siku 30.
Kazi hiyo ilimuingia Cristiano kiasi ambacho kwa Tsh ni 2,671,560,050 (Zaidi ya bilioni 2.6).
Lakini mktaba huu ulimhusisha Ronaldo peke yake, hivyo basi Real Madrid walisema jezi ya club yao isihusike wala promotion zao zisi-connect na club hiyo.
Kama vipi na wao ilibidi walipwe kwasababu brand yao ingetumika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni