STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 12 Februari 2016

STARTIMES LEAGUE KUMALIZIKA WIKIENDI HII

Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League) inatarajiwa kumalizika wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa kwa wakati mmoja katika viwanja mbalimbali nchini, huku Kundi A na C zikisaka vinara watakaopnda Ligi Kuu msimu ujao.
Bodi ya Ligi (TPLB) imeviandikia barua vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi hiyo, wasimamizi wa vituo kuwafahamisha kuwa mechi zote zinatakiwa kuchezwa kwa muda mmoja na kusisitiza kuwa mechi zote zitaanza saa 10 kamili jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.
Ni jukumu la Msimamizi na Kamishna kuhakikisha mechi yake inaanza katika muda uliotajwa (saa 10 kamili) bila kukosa. Utekelezaji wa maelekezo haya ni muhimu ikiwa ni moja ya njia ya kukabiliana na vitendo vyovyote vya upangaji wa matokeo vinavyoweza kujitokeza.
Mechi za mwisho za Kundi A hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Friends Rangers FC vs Kiluvya United FC (Mabatini), Polisi Dar vs Polisi Dodoma (Shirika la Elimu Kibaha), Ashanti United vs African Lyon (Karume) na Mji Mkuu vs Kinondoni Municipal Council FC zitachezwa Februari 14, 2016 katika viwanja husika.
Mechi za mwisho za Kundi B hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Kimondo Super SC vs Kurugenzi FC (Vwawa), Njombe Mji vs Lipuli FC (Amani), Ruvu Shooting vs Polisi Morogoro (Mabatini) na Burkina FC vs JKT Mlale (Jamhuri) zitachezwa Februari 13, 2016.
Mechi za mwisho za Kundi C hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Mbao FC vs Polisi Mara (CCM Kirumba), Polisi Tabora vs JKT Oljoro (Ali Hassani Mwinyi) na JKT Kanembwa vs Geita Gold (Lake Tanganyika) zitachezwa Februari 13, 2016 katika viwanja husika.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox