Edson Arantes do Nascimento sio jina geni katika medani ya soka na wengi tunamfahamu kwa jina la Pele ambae ni mchezaji wa zamani wa vilabu vya Santos ya nchini kwao Brazil na New York Cosmos ya nchini Marekani.
Kama ambavyo wengi tunamfahamu gwiji huyu wa soka katika tasnia ya soka akiwa kafanya mambo mengi makubwa na kushikilia rekodi kibao za soka kama ya kufunga magoli zaidi ya 1000 lakini pia akiwa na rekodi ya kuchukua kombe la Dunia mara tatu mwaka 1958,1962 na 1970.
Sasa katika mafanikio hayo ya soka yalio mwezesha kuchukua medani nyingi sana kipindi anacheza kabla ya kustaafu nguli huyu mzaliwa wa Três Corações, Minas Gerais, Brazil tarehe 23 October 1940 ameshtusha wengi mara baada ya kuamua kuvipiga mnada baadhi ya medani na zawadi mbalimbali alizo zipata katika soka.
Pele amedhamiria kuuza medani na baadhi ya vifaa vyake vya kimichezo 2000 kwa lengo la kupata fedha ili kusaidia Hospitali ya watoto iliyoko katika Jiji la Curitiba nchini Brazil inayofahamika kwa jina la Pequeno Principe children's hospital.
Mnada wa vitu hivyo utafanyika katika Jiji la London nchini Uingereza mwezi wa sita tarehe 7 hadi 9.
VITU AMBAVYO PELE ATAVIUZA
Jezi aliyo ivaa 1970-71
Mpira uliotumika katika mchezo wake wa 1000 kati ya Santos na Interland in 1971
Jezi ya klabu yake ya zamani New York Cosmos1975-77
Medani aliyopewa na klabu yake ya Santos FC,baada ya kushinda kombe la Dunia na taifa lake 1958
Kiatu cha Puma alicho vaa Pele in the 1970s.
Mpira ambao Pele alifunga goli la 1,000katika mchezo wa klabu yake ya Santos dhidi ya Vasco da Gama, ukichezwa Maracana Stadium , Rio
de Janeiro, Brazil November 19, 1969
A yellow and green satin sash with a
gold bullion fringe presented to Pele by the Brazilian Sport
Confederation to commemorate Brazil's legendary 1958 World Cup victory
Medani ya dhahabu katika kombe la Dunia 1962
Medani ambayo aliipata 1977 North American Soccer League (NASL) baada ya klabu yake ya New York Cosmos kushinda
A medal presented to Pele in 1954
after winning the 'Infanto Juvenil' championship while a member of Bauru
Atletico Clube Juniors
A rectangular silver
tone badge and attached blue ribbon worn by Pele, identifying him as a
member of the Brazil team during the 1958 World Cup held in Solna,
Sweden. The tournament was the scene of Pele's first
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni