Siku chache baada ya uchaguzi wa kumchagua Raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA kumalizika na muitaliano Gianni Infantino kushinda – leo imetoka taarifa juu ya mabadiliko ya sheria kadhaa zinazosimamia mchezo wa soka.
Imefahamika kwamba bodi ya kimataifa ya FIFA itabadilisha sheria ya kadi nyekundu na kuna uwezekano kukawa na mabadiliko pia katika kuongeza namba ya wachezaji wa kuingia kutoka kwenye benchi kufikia wanne – sheria ambayo inaweza kuanzia kwenye Euro 2016.
Baada ya mabadiliko ya kanuni ambayo yataanzia kwenye Euro 2016, kutakuwepo na sheria mpya juu ya faulo na kadi nyekundu.
Faulo dhidi ya mshambuliaji itakayotendwa na mchezaji wa mwisho wa safu ya ulinzi ya timu pinzani – sasa kosa hilo halitomfanya mchezaji kuadhibiwa kwa Kadi nyekundu ya moja kwa moja na kusimamishwa mechi 1, isipokuwa tu kama mcheza faulo atafanya vitendo vya vurugu au kushika mpira – na endapo faulo itakuwa ya kistaarabu ya kujaribu kuchukua mpira, basi refa atamuadhibu kwa kadi ya njano tu.
Kushika mpira sasa katikati ya mchezo sasa mtenda kosa hilo atapata adhabu ikiwa ataingilia mpira uliokuwa unaweza kuleta madhara upande wa timu yake.
Sheria nyingine ambayo inatajwa kubadilishwa ambayo bado haijathibitishwa – sheria inayohusu mabadiliko ya wachezaji dimbani.
Bodi ya kimataifa ya FIFA inafikiria wazo la kuruhusu mchezaji wa 4 badala ya watatu wanaoruhusiwa kufanyiwa mabadiliko kwenye mechi rasmi ya mashindano – ila tu endapo mechi hiyo itaenda kwenye muda wa ziada.
Kwa mujibu wa Calcio e Finanza, kuna uwezekano pia sheria itaruhusu mchezaji muda wote wa mechi na sio tu kwenye muda ziada huko baadae.
Uamuzi juu ya sheria hii bado unafanyia majadiliano kwa sababu unaweza kubadilisha sura ya mchezo wa soka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni