Mtanzania
Mbwana Samatta amezidi kuonyesha makali baada ya kufunga bao lake la
pili leo wakati KRC Genk ikishinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Oostende
katika mechi ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Samatta
amefunga bao la kwanza katika dakika ya 24 kwa kichwa likiwa ni la pili
kwake tokea ajiunge na timu hiyo akitokea TP Mazembe ya DR Congo.
Leon Bailey alifunga la pili katika dakika ya 39 na kuifanya Genk kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Leon Bailey alifunga la pili katika dakika ya 39 na kuifanya Genk kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Kipindi cha pili wageni waliendelea kucharuka lakini Genk iliendelea kuwa makini na kuendelea kuondosha hatari.
Genk ilipata mabao mengine mawili lakini tayari Samatta alikuwa ametoka katika dakika ya 74 na Igor de Camargo akaingia kuchukua nafasi yake.
Alejandro Pozuelo aliifungia Genk bao la tatu katika dakika ya 81 na Igor aliyeingia kuchukua nafasi ya Samatta akafunga la nne katika dakika ya 88 kabla ya wageni Oostende kufunga la kufutia machozi katika dakika za majeruhi kupitia Sebastiani Siani.
GOLI LA SAMATTA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni